Friday, 1 December 2017

Kumbe ZaiiD alishawishiwa na Ngwea kuachia Wowowo



Rapper wa SSK, ZaiiD amesema ngoma ya Ngwea ‘Singida Dodoma’ ilimshawishi kutoa ngoma yake inayobamba kwa sasa, Wowowo.
ZaiiD amesema licha ya Marehemu Ngwea kuwa na nyimbo nyingi zilizofanya vizuri lakini ngoma hiyo ni bora kwa upande wake.
“Singida Dodoma ni kama kamchezo tulikuwa tunakaimba huko utotoni na kaka zetu pia walikuwa wanaimba hivyo akipita binti wa hivyo lakini pia nimepata inspiration kwa Ngwea” amesema
“Hiyo ni ngoma ambayo aliitoka miaka ya nyuma haikuwa sana kama miziki yake mingine lakini mimi nilikuwa nikipenda, hivyo nikaona nimchukue kaka pale nimuingize kama sababu ametu-inspire watu wengi” amesema ZaiiD .

No comments:

Post a Comment