Thursday, 30 November 2017

Kampuni ya Dabaga yanunuliwa na kampuni ya Chai Bora



Katika kutekeleza sera ya uwekezaji nchini ili kuendana na kasi ya serikali ya kuwa na Tanzania ya Viwanda ifikapo mwaka 2025, kampuni ya Chai Bora imeinunua kampuni ya Dabaga iliyokuwa ikitamba na bidhaa za kuongeza ladha za vyakula kama vile Dabaga tomato sauce , Pilipili Mbuzi, Mango pickle na bidha nyinginezo.

Kampuni ya Chai Bora imekuwa ikifanya shughuli zake hapa nchini tangia mwaka 1990, Chai Bora inaogoza kama chata ya kuzalisha majani ya chai, Ikijikita zaidi katika uzalishaji wa bidhaa kama vile majani kama vile Black Tea, Green Tea pia Kahawa aina ya Café Bora. Kwa kuwa imeanza kazi tangia mwaka 1990 hadi sasa ni takribani miaka 27 inaashiria ukuaji katika sekta husika ya bidhaa za Chai . Katika hiyo miaka 27 Chai Bora imeinunua kampuni ya Dabaga, imeongeza uzalishaji wa bidhaa tofauti na imeboresha kiwanda cha Dabaga Iringa na teknolojia za kisasa.

Uwekezaji huo ambao umehusisha teknolojia za kisasa na mitambo ya kisasa zaidi ni wazi kuwa itaongeza ufanisi kwenye uzalishaji wa bidhaa husika na kusukuma ongezeko la ajira nchini. Kupitia uzalishaji huo kwa sasa kiwanda hicho kimetoa ajira ya moja kwa moja na ajira isiyokuwa ya moja kwa moja kwa wakazi wa kijiji cha Ikokoto cha wilayani Ilula, Iringa. Wakulima ambao wanaojihusisha na shughuli za malighafi za viwanda kama hicho hasa wakulima, wasambazaji wa bidhaa za kilimo pamoja na watoa huduma wengine kama vile kampuni za ulinzi, usafi na hata watoa huduma za vyakula nao watanufaika na uwekezaji huo.

Mkurugenzi wa Chaibora, Mr.Kapila Mr.Kapila Ariyatilakakaalisema wakulima watanufaika kwa kuuza mazao yao hasa nyanya kwa kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinahitaji nyanya tani 300 hadi 400 kwa mwezi. "Hii inaashiria kuwa wakulima wa nyanya wa ndani na nje ya Iringa watanufaika na uwepo wa kiwanda hicho hasa kwa kuuza bidhaa zao humo" anasema Mr.Kapila Ariyatilaka.

Anasema wasambazaji wanaojihusisha na bidhaa za kilimo nao wamepata mwanya wa kuuza bidhaa zao na hasa wanaweza kununua kwa wakulima na kisha kuuza kwenye kampuni hiyo na hivyo kuongeza wigo wa ajira.

No comments:

Post a Comment