Harare, Zimbabwe. Mchungaji mwanaharakati Evan Mawarire aliyeshtakiwa mahakamani kwa jaribio la kutaka kumpindua Robert Mugabe wakati wa mgomo uliodhoofisha usafiri katika miji yote mikubwa amefutiwa mashtaka.
Uamuzi huo umekuja wiki moja tangu Mugabe, aliyetawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, alipojiuzulu kutokana na shinikizo la jeshi.
"Hakuna ushahidi kuthibitisha kwamba yeye (Mawarire) alihimiza machafuko ya kuiondoa serikali," alisema katika hukumu yake Jaji wa Mahakama Kuu Priscilla Chigumba.
Jaji alisema Mawarire alihimiza mgomo usio na machafuko yakiwa ni majibu kutokana na mgogoro wa kiuchumi.
Mawarire aligeuka na kuwa taswira ya maandamano ya kumpinga Mugabe mwaka jana aliposambaza video yake katika wavuti akiwa amejifunga bendera ya taifa huku akilalamikia matatizo ya Zimbabwe.
Video hiyo ilitumika kushawishi vuguvugu lililoitwa BenderaHii na kusababisha migomo nchi nzima. Serikali ilijibu kwa kupiga marufuku maandamano ya mitaani jijini Harare katika kile ilichoita ni “matumizi mabaya” ya bdenera.
"Safari nzima imekuwa upuuzi," Mawarire aliwaambia wanahabari.
"Sikuwa mtu wa kupandishwa kizimbani. Sikutakiwa hata kutumia miezi 11 nikijaribu kujitetea juu ya haki zangu kikatiba,” alisema.
Pia Manawire amemuonya rais mpya Emmerson Mnangagwa, veteran wa chama tawala cha Zanu-PF kwamba asithubutu kukaba koo haki za watu.
No comments:
Post a Comment