Dodoma. Vijana wametakiwa kufanya siasa za kistaarabu na wajikite katika ujasiriamali.
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ametoa rai hiyo leo Jumatano Novemba 29,2017 alipofungua mkutano wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dodoma.
Pinda amesema siasa bila kujishughulisha zinakosa tija na matokeo yake ni vijana kuishia kulalamika.
Pia, amezungumzia suala la vijana kuhama CCM akisema wanapotea. Amewataka kutulia kwa kuwa wataweza kupaza sauti zao.
Pinda amewataka wagombea kuwa kitu kimoja na kushirikiana na watakaoshinda kwa kuwa huo ndiyo msingi wa CCM.
No comments:
Post a Comment