Thursday 2 November 2017

Jela miezi 6 kwa kuoa mke wa pili Pakistan




Mahakama nchini Pakistan imemfunga mwanamume mmoja miezi sita jela ya kuoa mke wa pili bila ya idhini kutoka kwa mke wake.

Mahakama hiyo ya mjini Lahore pia ilimuamrisha Shahzad Saqib, kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne.

Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha Bibi, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan.

Wanaharakati wa masuala ya wanawake wabasema kuwa kesi hiyo ni pigo kwa ndoa za wake wengi.
Mfasiri wa FBI afunga ndoa na mwajiri wa IS

Pia walisema kuwa itawapa wanawake zaidi walio katika hali kama hizo motisha ya kupeleka kesi mahakamani.

Nchini Pakistan, wanaume wanaotaka kuoa wanawake kadhaa hufanya hivyo baada ya miaka kadhaa na ni lazima wapate idhini kutoka kwa mke wa kwanza.

Baraza la kiislamu nchini Pakistan ambalo hutoa ushauri wa serikali kuhusu masuala ya kiislamu, mara kwa mara limekosoa sheria za familia nchini humo.

Sadiq ana haki ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo ya siku ya Jumatano.

No comments:

Post a Comment