Tuesday, 31 October 2017

Mwakibinga amfananisha Zitto Kabwe na Harmorapa




KIJANA kutoka Kundi la Vijana Wazalendo nchini, James Mwakibinga, amekuja juu na kumshukia kiongozi wa Chama cha Act- Wazalendo, Zitto Kabwe na kusema anatafuta kiki kama Harmorapa kwa kupingana na kasi ya Rais Dk .John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi uliofanyika katika madini nchini.

Mwakibinga amesema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa mambo yanayofanywa na kiongozi huyo siyo ya kizalendo na hayafai kufumbiwa macho na mtu yoyote mwenye akili na mwenye dhamira ya kweli kwenye taifa lake.

“Nadiliki kusema kuwa game changer amebadilisha mchezo hivyo wanasiasa wanashindwa kufanya kazi katika majimbo yao na kazi yao imekuwa kufanya upotoshaji  juu ya kazi zilizofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli hasa katika swala zima la kuokoa mali za Watanzania katika sekta ya madini,” amesema Mwakibinga.

Amesema Zito anatakiwa kufanya siasa za kistaarabu na kuacha kupayuka tu kwani hii ni miaka miwili bado mitatu hivyo zama hizi zimebadilika hakuna utaratibu tena wa mashirika kuwahonga viongozi wa kisiasa.

Mwakibinga amesema kuwa vijana wazalendo wako nyuma yake watamlinda na kusimamia misingi yote ya kulinda rasilimali za wananchi zisiendelee kuibwa.

No comments:

Post a Comment