Thursday, 2 November 2017

Basi lagonga kichwa cha tren




Kada Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma amewasihi Watanzania kumpuuza Mwanasiasa Lazaro Nyalandu ambaye juzi ametangaza kujivua nyadhifa zake zote katika CCM ikiwemo ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa kile alichodai Serikali kukigandamiza Chama na CCM kupoteza mwelekeo.

Lusinde amesema Bw. Lazaro Nyalandu hakuwahi kunyimwa nafasi yoyote ya kutoa maoni yake ama dukuduku zake ndani ya chama wala bungeni na kwamba uamuzi huo unaashiria kuwa anatafuta kinga ya kutochukuliwa hatua kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili.

Kada huyo wa CCM amesema ana wasiwasi ndani ya Serikali wapo watendaji ama viongozi wasio waaminifu ambao watakuwa wamevujisha taarifa za hatua ambazo Serikali inatarajia kuzichukua dhidi kutokana na makosa makubwa aliyoyasababisha alipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na alipokuwa Naibu Waziri

No comments:

Post a Comment