Wadau kutoka sekta mbalimbali wafurahishwa na kasi ya maendeleo inayoletwa na Rais Magufuli
Ikiwa imetimia miaka miwili ya rais Magufuli tangu aingie madarakani kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wananchi,wadau kutoka sekta mbalimbali nchini wameonesha kuridhishwa na kasi ya rais Magufuli katika maendeleo inayohusisha utendaji kazi wake pamoja na msimamo thabiti anaouonesha katika kulinda rasilimali za nchi ili kuwanufaisha watanzania walio wanyonge na masikini.
Hayo yamebainika kwa kutoka kwa wakazi waliopo jijini Dar es Salaam na pembezoni ambapo pamoja na mambo mengine wakazi hao wanaridhishwa na namna serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli inavyojitoa katika kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi haraka tofauti hapo awali huku wengine wakianisha mambo ambayo rais Magufuli ameyatekeleza kwa haraka ndani ya miaka miwili ilihali ya kwamba bado ana miaka mingine mambo hayo ikiwa ni elimu bure,madawati,ujenzi wa miundombinu,kuokoa fedha zilizokuwa zikilipwa kwa watumishi hewa.
Aidha,kutokana na uchapakazi wake katika vita vya kiuchumi na kutaka kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda wananchi hao wamesema ni dira njema ya kuleta mafanikio kwa taifa hivyo rais Magufuli aendelee na juhudi zake za kutosikiliza maneno ya wale wanaopinga juhudi hizo.

No comments:
Post a Comment