Sunday, 29 October 2017

Goli la Kichuya lanunuliwa kwa Tsh. 500,000

Mashabiki wa Simba kundi la Simba Kwanza (SK) wamekabidhi shilingi 500,000 Shiza Kichuya baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’ ikiwa ni kutokana na goli alilowafunga watani wao wa jadi mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Mashabiki hao wamemchagua Kichuya kuwa Man of the Match wakiwa wameridhishwa na kiwango alichokionesha kwenye mchezo huo.

Kichuya aliifungia Simba bao la kuongoza lakini baadae goli hilo lilisawazishwa na Obrey Chirwa na kulazimisha timu hizo za Kariakoo kugawana pointi.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo amesema, huo utakuwa ni utaratibu wao wa kila mechi kutoa zawadi ya pesa kwa mchezaji atakaefanya vizuri kwenye mechi.

Ameahidi kuwa, mechi ijayo ya Simba (Mbeya City vs Simba November 5, 2017) watatoa kisasi cha shilingi 2,000,000

No comments:

Post a Comment