Tuesday, 31 October 2017

Kiongozi wa Catalonia aliyefutwa "aenda Ubelgiji"



Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema.

Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi.

Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku.

Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa.

Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita.

Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.

Mbona Puigdemont akaenda Ubelgiji?
Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba.

Serikali ya Ctalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya wapiga kura walishiriki huku asilimia 90 ya wapiga kura hao wakiunga mkono uhuru

Siku ya Ijumaa bunge la Catalonia likatangaza uhuru, Kisha waziri mku wa Uhispania akatangaza kuvunjwa kwa bunge la eneo hilo na kuondole kwa Bw. Puigdemont kama kiongozi wa Catalonia.

No comments:

Post a Comment