Friday, 3 November 2017

Waziri Nchemba ameonekana mazoezi ya Singida Utd kulekea mechi vs Yanga




 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba ambaye ni mdau mkubwa timu ya Singida United leo Ijumaa asubuhi alikuwepo kwenye mazoezi ya mwisho ya timu hiyo kwenye uwanja wa Namfua Singida kuelekea mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga.

Waziri Nchemba amekuwa karibu na Singida United tangu ikiwa ligi daraja la kwanza, baada ya timu hiyo kupanda kucheza VPL kwa mara nyingine baada ya muda mrefu bado amekuwa akionekana viwanjani kuisapoti kwa karibu.

Kumbuka kuwa, Waziri Nchemba ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (Singida) mahali ambapo ni nyumbani kwa Singida United.

Waziri Nchemba pia alipiga penati kadhaa katika mazoezi hayo ya mwisho ambayo yalishuhudiwa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambayo wataishuhudia kwenye uwanja wao wa nyumbani Namfua mjini Singida.

Uwanja wa Namfua utakuwa ukitumika kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu, Singida United walikuwa wakiutumia uwanja wa Jamhuri Dodoma kupisha ukarabati wa uwanja wa Namfua.

Kwa mujibu wa Ibrahim Mohamed maneja wa Singida United, Nizar Khalfani ndio mchezaji pekee mwenye majeraha ambaye hajafanya mazoezi ya mwisho ya pamoja kwa hiyo ataukosa mchezo wa kesho.

“Nizar Khalfani ndio mchezaji pekee ambaye hata kuwa sehemu ya mechi ya kesho kwa sababu anasumbuliwa na majeraha, wachezaji wengine wote wako vizuri kabisa na wamefanya mazoezi ya pamoja.

No comments:

Post a Comment