Sunday, 29 October 2017

Milipuko miwili yatokea mji mkuu wa Somalia

Milipuko miwili imetokea mjini Mogadishu nchini Somali chini ya wiki mbili baada ya shambulio kubwa la bomu kuwaua watu 350.

Mlipuko wa kwanza ulitokea baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kuvurumishwa na kuingizwa kwa nguvu hotelini.

Wanamgambo wenye silaha kisha walifuata na kuingia ndani ya jengo hilo.

Milio ya risasi ingali ikiendelea kusikika ndani ya hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, ambao ulishambuliwa na kundi la kigaidi la kiislamu, la Al- Shabaab. Yamkini watu 17 wanasemekana kuuwauwa kufikia sasa. Wanamgambo hao wanasemekana kuvamia jumba la Hoteli hiyo, mara tu baada ya mabomu mawili kulipuka nje ya majengo hayo.

Duru zinasema kuwa watu kadhaa wamepigwa risasi ndani ya hoteli hiyo, wakiwemo watoto na mbunge mmoja wa zamani.

Hoteli hiyo ilipangiwa kuandaa mkutano wa kiusalama leo Jumapili.

Majuma mawili yaliyopita, mji wa Mogadishu, ulikumbwa na shambulio baya zaidi la bomu kuwahi kutokea nchini Somalia, amabapo zidi ya watu 350 waliuwawa.

Mlipuko wa pili ulitokea karibu na majengo ya zamani ya bunge ambayo yamo hapo karibu.
Bado haijabainika idadi ya waliofariki.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabaab ambalo lililaumiwa kwa shambulio hilo la wiki mbili zilizopita, ingawa halikujitokeza kukiri, limejitokeza na kusema lilitekeleza mashambulio hayo ya leo.

Afisa wa polisi Mohamed Hussein ameambia shirika la habari la Reuters kwamba: "Watu zaidi ya saba wamefariki wakiwemo wanajeshi na raia."

Shirika la huduma ya dharura la Aamin mjini humo limesema tayari limesafirisha majeruhi 15 hadi hospitali na kwamba kulikuwa na "miili mingi ya waliofariki".

Afisa wa polisi Ibrahim Mohamed ameambia AFP kwamba katika mlipuko wa pili, gari lililokuwa limejazwa vilipuzi lililipuka karibu na makutano ya barabara.

Shambulio hilo limetekelezwa huku viongozi wa mkoa wakikutana mjini Mogadishu kwa mkutano Jumapili kukubaliana kuhusu mkakati wa pamoja wa kukabiliana na al-Shabab.

Shambulio lililotekelezwa tarehe 14 Oktoba lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 358.
Watu 56 bado hawajulikani walipo

No comments:

Post a Comment