Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki(CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua.
Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi amempongeza Nyalandu kwa kuwa ni alikuwa mbunge jirani yake na kuwa ujasiri wa kufanya hivyo.
Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia uchaguzi wa madiwani katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini.
“Kuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka,”amesema Lissu leo Jumanne akiwa jijini Nairobi
No comments:
Post a Comment