Ni mara chache sana kusikia kiongozi au hata shaki wa Simba na Yanga kusifia timu pinzani kutokana na utamaduni wa vilabu hivyo ulivyo hata kama watatakiwa kupongeza, leo October 31, 2017 Haji Manara amesema waziwazi kukubali mbinu zilizotumiwa na kocha wa Yanga George Lwandamina kwenye mchezo wa Yanga vs Simba Jumamosi iliyopita.
Manara amesema Lwandamina ni mtu wa mbinu na alifanikiwa katika mbinu zake za kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1, Simba walianza kupata goli la kuongoza lakini Yanga wakasawazisha dakika mbili baadaye.
“Yanga walicheza vizuri tena kwa nidhamu, kocha wao ni mtu wa mbinu sana alikuja kupaki ‘basi’ kwa heshimba ya kuiheshimu Simba lakini akazitumia vizuri ‘counter attack’, walicheza vizuri bila shaka kwa sababu walikuja kama underdogs wakatuheshimu, wakapaki basi lao vizuri.”
Manara amewaambia Yanga kwamba, kushangilia kwao matokeo ya sare ya 1-1 yanadhihirisha Simba ni klabu kubwa Tanzania.
“Yanga ni imu kubwa, hamuwezi kwenda kucheza na Simba kamawanyonge lakini baada ya matokeo ya 1-1 wakashangilia na hiyo ndiyo inayonipa tatu. Tuliwazidi umiliki wa mpira 58% kwa 42%. Sisi hatukuridhika kutoka sare na Yanga na hatutaridhika kutoka sare na timu yoyote Tanzania kwa sasa hivi kwa sababu tuna kikosi kizuri.”

No comments:
Post a Comment