Mwigizaji na msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi maarufu kama ‘Ray’, amewaongoza mashabiki wa Yanga SC kutoka kundi la ‘Yanga For Life’ kwenye mtandao wa WhatsApp kutoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo.
Ray na wenzake wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘Shin Gard’, mchana wa leo kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.
Miongoni mwa wachezaji waliopata zawadi hizo ni mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili za Kagera Sugar na Stand United.
Kiungo kutoka DRC Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye aliibuka nyota wa mchezo wa watani wa Jadi jumamosi iliyopita amepewa zawadi ya shilingi laki tano huku kipa Youthe Rostand, akipata shilingi laki mbili, viatu na ‘Shin Gard’.
Baada ya kukabidhi zawadi hizo Ray amesema nia ya kundi lao ni kuwapa hamasa wachezaji wao ili waweze kutetea ubingwa wao wa ligi na kutwaa mara ya nne mfululizo
No comments:
Post a Comment