Friday, 3 November 2017

Republican wabuni mbinu za marekebisho ya kodi

Wanachama wa Republican nchini Marekani wamebaini mpango wa marekebisho ya kodi kubwa kwa kipindi cha miaka 30 ijayo.

Marekebisho hayo ya kodi, yamekuwa kipaumbele cha ajenda za Rais Donald Trump.
Mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja na kupunguza kodi katika biashara kutoka asilimia 35 hadi asilimia 20 na kupandisha posho binafsi ya kodi.

Marekebisho mengine yaliyopendekezwa ni kuondoa viwango vya kodi katika magari ya umeme, hali itakayo waathiri watengenezaji wa magari kama vile kampuni ya general Motors,Tesla na Nissan.

Mpango huu wa Republican ambao unapaswa kuidhinishwa na bunge Congress, unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa deni la taifa

No comments:

Post a Comment