Tuesday, 17 October 2017

Wachezaji Wa Yanga waliokuwa wamebaki Dar waongeza nguvu tabora,,,,

Klabu ya soka ya Yanga itaungana na wachezaji wake waliokuwa wamebaki jijini Dar es salaam wakati timu imesafiri kwenda mkoani Kagera kucheza na Kagera Sugar wikiendi iliyopita.
Yanga tayari imeshatoka Kagera na kutua mkoani Tabora ikijiwinda na mchezo wake wa ligi kuu raundi ya 7 dhidi ya Stand United utakaopigwa wikiendi ijayo mjini Shinyanga.
Meneja wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Hafidh Saleh amewataja wachezaji hao kuwa ni Juma Mahadhi, Pato Ngonyani, Ramadhan Kabwili, Abdallah Hajji, Juma Mahadhi na Saidi Mussa.
Aidha meneja Saleh amesema kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi ambao ni Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Amisi Tambwe wataendelea na mapumziko hadi timu itakaporejea jijini Dar es salaam.
Kesho Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kwenye uwanja wa Al Hassan Mwinyi kabla ya kuelekea mjini Shinyanga kucheza na Stand United

No comments:

Post a Comment