Sunday, 15 October 2017

Bodi mpya ya ligi kuu kujulikana leo

Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo inatarajiwa kupata viongozi wapya kufuatia uchaguzi mkuu utakaofanyika leo Oktoba 15 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salam.
Jumla ya wajumbe 44 wanashiriki Mkutano huo wa uchaguzi wa Baraza Kuu la TPLB. Wajumbe hao ni klabu 16 za Ligi Kuu, klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na wawakilishi wanne wa klabu za Ligi Daraja la Pili.
Wanaowania nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB ni Clement Andrew Sanga kutoka Yanga na Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar. Nafasi ya makamu mwenyekiti inawaniwa na Shani Christoms Mligo wa Azam FC.
Nafasi tatu za kuwakilisha klabu za Ligi Kuu kwenye Kamati ya Uongozi zinawaniwa na wagombea wawili ambao ni Hamisi Mshuda Madaki (Kagera Sugar) na Ramadhani Marco Mahano (Lipuli).
Almasi Jumapili Kasongo kutoka Ashanti United FC amejitokeza kuwania nafasi ya uwakilishi wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Wakati Edgar William Chibura kutoka Abajalo FC anawania nafasi ya uwakilishi ya klabu za Ligi Daraja la Pili kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB.

No comments:

Post a Comment