Sunday 15 October 2017

RC Gambo Amesema hana mpango Wa kugombea ubunge mkoa Arusha,,,,,

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema hana mpango wa kugombea ubunge Arusha Mjini ila anachofanya sasa ni kutekeleza ahadi za Rais John Magufuli za kutatua kero za wananchi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Gambo alisema wanaosambaza uvumi kuwa atagombea ubunge ni wanasiasa ambao hawajiamini na wameshindwa kutatua kero za wananchi.
“Kazi ambazo nafanya kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wakuu wa wilaya ni kutatua kero na tumeachana na mambo ya kisiasa, sisi tunachapa kazi,” alisema.
Alifafanua kuwa baadhi wabunge hawaonekani majimboni na kuwaachia viongozi wa Serikali kufanya kazi zilizopaswa kufanywa na wabunge.
Akizungumzia tuhuma za kununuliwa madiwani wa Chadema zilizotolewa na wabunge wa chama hicho, alisema anaamini hakuna masuala ya rushwa.
Gambo alisema madiwani hao wamejiuzuru baada ya kuridhishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais Magufuli.
“Kuna madiwani wa Arusha, Monduli, Ngorongoro, Arumeru, Hai, Iringa na maeneo mengine hawa wote wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano,” alisema.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro alisema wilaya hiyo imefanikiwa kutatua kero za wananchi ikiwamo upatikanaji wa huduma muhimu.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza katika shughuli ya uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa

No comments:

Post a Comment