Sunday, 15 October 2017

Waziri Mwigulu : Tutahakikisha sheria inabadilishwa,,,,,,,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wizara yake itahakikisha inawabana ipasavyo wahamiaji haramu pamoja na kubadilisha sheria ili ziwabane zaidi.
Waziri Mwigulu ameyasema hayo alipotembelea Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo na kugundua robo tatu ya wafungwa ni wahamiaji kutoka nchi jirani ikiwemo Ethiopia.
Taarifa ya Mkuu wa magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, SACP Boyd Mwambingu imebainisha kuwa wafungwa ambao ni raia wa Ethiopia waliofungwa katika Magereza ya Mkoa huo ni 334, Mahabusu 12 na wanaosubiri kusafirishwa ni 91 ambao jumla ya raia kutoka Etheopia ni 437 wa Malawi ni 1 Msomali ni 1 wa DRC ni 1 wa Burundi 2 na Kenya ni 2.
Kufuatia taarifa hiyo Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema haiwezekani wahamiaji haramu wagharamikiwe na taifa ikiwemo kusafirishwa kwa gharama za serikali pamoja na kupatiwa Chakula na Matibabu.
“Tutafanyia kazi ili sheria iseme kama watakamatwa watafungwa au mambo mawili, nchi yao iwachukue au warudi kwa gharama zao wenyewe lakini sheria lazima iwe kali itakayotoa fundisho kwa wengine”, amesema Mwigulu.

No comments:

Post a Comment