Thursday, 19 October 2017

Wema Sepetu na wasanii wengine wamfaliji Lulu

Dar es Salaam . Msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliomfariji Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia iliyoanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Wasanii wametumia mtandao wa Instagram kumfariji mwigizaji Lulu ambaye ni mshindi wa tuzo za filamu za AMVCA.
Jackline Wopler, Katarina Karatu, Nisha, Aunt Ezekiel na wengine wametuma picha za mwigizaji huyo zikiambatana na maneno ya kumfariji wakimweleza kuwa atavuka salama katika mtihani huo.
Kupitia ukura wake wa Instagram, Wema ameweka picha ya Lulu na kuandika, “This Too Shall Pass Baby… God is Great u know… so have faith… ur in my prayers,” akiwa na maana hata hili litapita, Mungu ni mkubwa hivyo anatakiwa kuwa na imani na atamwombea.
Lulu anadaiwa Aprili 7,2012 alimuua bila ya kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Kesi inasikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

No comments:

Post a Comment