Thursday, 19 October 2017

Kauli ya Ridhiwani kikwete kuhusu Tundu Lissu,,,,

Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amefunguka na kusema kuwa amefurahi kumuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa mwenye tabasamu na furaha na kuzidi kumuombea apone kabisa na kurudi kupambana.
Ridhiwani Kikwete amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema Mungu siku zote anatenda wema kwa watu kufuata kushambuliwa kwa risasi nyingi Tundu Lissu na hatimaye kuweza kupona na sasa furaha yake kuanza kurejea.
"Mungu utenda wema siku zote. Ashukuliwe yeye kwa kazi ya kurejesha tabasamu katika sura yako na afya kwa wanaokuuguza. Nimefurahi kukuona tena msomi, Kiongozi wangu na mwana kamati mwenzangu wa Bunge ukitabasamu na mwenye Afya njema. Mungu akulinde na akusimamie katika matibabu yako .Looking forward to see you back into your good shape" aliandika Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma na kisha baadaye kusafirishwa na kupelekwa jijini Nairobi Kenya kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu

No comments:

Post a Comment