Monday, 16 October 2017

Austria kumchagua kiongozi mwenye umri mdogo zaidi duniani,,,,,

Mkuu wa chama cha kihafidhina nchini Austria cha People's Party, Sebastian Kurz, anaelekea kuwa kiongozi wa taifa mwenye umri mdogo duniani, baada ya ushindi wake katika uchaguzi mkuu hapo jana.
Kurz aliye na umri wa miaka 31 amepungukiwa na uwingi , lakini yupo katika nafasi nzuri ya kuunda serikali ya muungano.
Haijulikani wazi iwapo atafikiria kuunda serikali ya muungano na chama kinachopinga uhamiaji Freedom Party, kilichoibuka nafasi ya tatu kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Akihutubia wafuasi wake Bw Kurz alisema: "Ni wakati wa kuleta mabadiliko kati nchi hii. Leo ni siku muhimu kwetu kuibadilisha nchi hii na ninasema asante kwa wale wamewezesha hili".
"Nina furaha, nimejitolea kuifanyia kazi Austria."
Sebastian Kurz ni nani?
Kabla ya uchaguzi Bw. Kurz lihudumu kama waziri mwenye umri mdogo zaidi wa mashauri ya nchi za kigeni barani ulaya, baada ya kuteuliwa mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 27.
Mwezi Mei mwaka 2017 akawa kiongozi wa chama cha People's Party. Alianza taaluma yake ya siasa katika tawi la vijana wa chama kabla ya kwenda kuhudumu katika baraza la manispaa la mji wa Vienna.
Akipewa jina "Wunderwuzzi" linalomaanisha mtu anayeweza kutembea juu ya maji, amefananishwa na viongozi vijana wa Ufaransa na Canada, Emmanuel Macron na Justin Trudeau.
Sawa na Macron, Bw Kurz amejiundia wafuasi wanaomzunguka, kukibadilisha chama cha People's Party, ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 30

No comments:

Post a Comment