Tuesday 17 October 2017

Meya wa Kinondoni atoa sababu 3 za kusaini mkataba na CRJE

Meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamin Samweli Sita leo amesaini mkataba wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata takataka na kuwa mbolea kitakachojengwa na kampuni ya CRJE ambapo ujenzi huo unatarajia kuanza kesho.
Meya Sita amewaeleza waandishi wa habari kuwa sababu ya kusaini mkaba huo ni kwamba mbolea aina ya mboji itakayozalishwa na kampuni hiyo haitaharibu udongo kwani tofauti na njia ambayo imezoeleka ya Chemical Fertilizer ambayo inaharibu udongo kwa kiasi kikubwa.
Pia amesema kujengwa kwa kiwanda hicho kitaongeza ajira kwa wananchi pia kitawasaidia wakulima kutumia mbolea ambayo ni bora na ya kisasa huku ikiwa haina athari kwa udongo na hata mazao.
Aidha kupitia mkataba huo manispaa ya Kinondoni itakuwa imeunga mkono kiasi kikubwa jitihada za Rais Magufuli katika kuelekea Tanzania ya viwanda, hivyo wananchi watapata ajira mbalimbali za kutoka kiwanda hicho.


No comments:

Post a Comment