Monday 16 October 2017

Ibrahim Ajib Namba 10 Amekuja yanga wakati muafaka,,,

WAKATI mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC walipoichapa KageraSugar FC 2-1 katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba Jumamosi iliyopita na ‘kufunga’ gepu la pointi na viongozi wa ligi, kiungo-mshambulizi, Ibrahim Ajib ameendelea kuwathibitishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa hahitaji sana muda ili kuanza kuwaonyesha ‘thamani’ yake.
Yanga ilikuwa timu pekee kati ya 16 kupata ushindi katika michezo ya mzunguko ya sita na alama hizo tatu walizozipata ugenini zimewafanya kufikisha pointi 12 sawa na Simba SC, Mtibwa Sugar FC na Azam FC ambao wote walishindwa kupata ushindi wakati michezo saba ya raundi hiyo ilipomalizika kwa matokeo ya sare/suluhu.
Magoli matatu ya Ajib, pointi 9 za Yanga
Yanga imeangusha pointi mbili tu katika michezo mitatu waliyocheza ugenini hadi sasa. Wamefanikiwa kufunga katika viwanja vya Sabasaba, Njombe (goli moja), Majimaji, Songea (goli moja) na wikendi iliyopita walipandisha kiwango chao kiufungaji kwa mara ya kwanza msimu huu walipofanikiwa kutikisa nyavu za golikipa Juma Kaseja mara mbili.
Ajib amehusika katika magoli matatu kati ya manne ambayo timu yake imefunga ugenini, huku akiongoza chati ya ufungaji katika kikosi hicho cha kocha Mzambia, George Lwandamina akiwa na magoli matatu kati ya sita ambayo timu yake imefanikiwa kufunga katika michezo sita iliyopita katika VPL.
Alifunga goli lake la kwanza akiwa mchezaji wa Yanga na kuisaidia timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC. Goli hilo ni la kwanza la mpira uliokufa msimu huu. Akafunga tena katika ushindi wa 1-0 vs Ndanda FC katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Na sasa ametoka kufunga goli lake la tatu katika michezo sita ya ligi kuu, huku akipiga pasi ‘ya video’ kwa Obrey Chirwa aliyefunga goli la kwanza vs Kagera Sugar.
Hadi sasa Ajib amekuwa na mchango mkubwa sana katika kikosi cha Yanga hasa wakati huu ambao safu yao ya mashambulizi inatetereka kutokana na majeraha ya mara kwa mara yanayowaandama, Mrundi, Amis Tambwe, Mzimbabwe, Donald Ngoma na Chirwa.
Kuendelea kwake kufunga magoli kunaipa nafasi timu yake kuendelea kupanda juu kimsimamo kwani licha ya kufunga magoli sita tu katika michezo sita iliyopita ila safu ya ulinzi imekuwa imara na hata magoli matatu waliyoruhusu hadi sasa hajawaathiri sana.
Ajib ni namba 10
Uwepo wa Pius Buswita katika kikosi cha Yanga hivi sasa kumekumeongeza ufanisi wa timu katika utengenezaji wa nafasi. Buswita anaenda sana kurahisisha mpira kwa pasi zake zake fupifupi za ‘one-two’. Katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kocha Lwandamina aliwapanga washambuliaji wawili-Ajib na Chirwa.
Upande wa kushoto alimpanga Geofrey Mwashuiya, Buswita akawa anaibia katika wing ya kulia-huku akisogea sana katikati wakati wakishambulia ili kumpa nafasi beki namba mbili Juma Abdul kupanda kwa ajili ya kupiga krosi pasi.
Ajib alikuwa akipata uhuru wa kushuka hadi eneo la kati la kuichezesha timu kama vile ni kiungo mchezeshaji, alipiga pasi ya juu ya kupenyeza akitokea na mpira eneo la kati na mpira ule aliuchopu na ukaangukia nyuma ya walinzi wa Kagera Sugar, Juma Nyosso na patna wake Juma Shemvuli, na kitendo cha wao kugeuka wakamkuta tayari Chirwa anautazama mpira uliodondoka mbele yake huku golikipa Kaseja akisubiri nini atafanya.
Nimeandika makala kadhaa na nimekuwa nikisisitiza Lwandamina anapaswa kutumia washambuliaji wawili wa kati wakati huu ambao nyota wake wa mashambulizi wakipambana na majeraha. Na faida niliyokuwa naitaraji ndiyo ile ambayo Ajib alionyesha. Kupiga pasi za mwisho zisizotarajiwa akitokea kati mwa uwanja, na kufunga magoli muhimu.
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kagera Sugar naamini sasa, Lwandamina atakuwa amemshuhudia namba kumi bora ambaye anaweza kucheza vizuri sambamba na Chirwa au Tambwe ambao wanauwezo mkubwa wa kusimama na kutengeneza nafasi wakicheza kati zaidi. Hakika Ajib tayari ameanza kujibu matarajio ya wengi ambao waliamini angeweza kuyafanya baada ya kusajiliwa kutoka Simba msimu huu.
Alicheza akimzunguka Chirwa huku akili yake akionyesha kuwa na haraka katika kufikiria, huku akifikia maamuzi ya hatari kwa kila pasi yake iliyoelekea golini kwa timu pinzani. Aligusa mpira kiufundi, huku kiwango chake cha utendaji kazi kikiwa juu. Huyu ni namba 10 sahihi aliyekuja Yanga katika wakati mwafak

No comments:

Post a Comment