Friday 20 October 2017

Uongozi wa Trump wakosolewa na Marais hawa

Marais wa zamani George Bush na Barrack Obama
Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.
Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.
Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey.
Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.
Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.
Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.
Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika ikulu ya Whitehouse.
lakini maadili na viwango vya tabia ambazo awali zilikuwa zikifuatwa sasa zimesahaulika katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersy, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.
Aliongezea: Kile ambacho hatufai kuendelea nacho ni kuwa na siasa za zamani za kugawanyana ambazo zimekuwepo nyakati za wali.
Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma.Ni karne ya 21 sio 19. jamani!.

No comments:

Post a Comment