Sunday, 15 October 2017

Mourinho: sikwenda Anfield kumburudisha mtu yeyote bali tulikwenda kucheza soka.

Msimu wa ligi kuu Uingereza wakati unaanza kila mtu alimsifu Jose Mourinho kwa kuibadilisha United, walionekana wanacheza soka la kuvutia sana tofauti na msimu wa mwaka juzi.
Lakini baada ya mechi 7 ambazo hawakucheza na timu ngumu sana, jana United walipata kipimo chao cha kwanza baada ya kukanyaga katika uwanja wa Anfield kucheza dhidi ya majogoo wa London Liverpool.
Mambo yalibadilika na United walicheza ambavyo hakuna aliyetarajia, wakawa United wale wale wa kurudi nyuma kusubiri mipira ije huku wakiwaacha Liverpool kuushikilia mchezo wote.
Baada ya mchezo huo kuisha sasa sio mashabiki tu bali hata wachambuzi wa soka walianza tena kubeza mfumo wa kocha Mourinho dhidi ya timu kubwa na kudai kwamba unaboa sana kuangalia kama walivyocheza jana.
Mourinho mwenyewe amewaambia wanaoponda kwamba kila mtu auchukulie huo mchezo auchukuliavyo na hakwenda Anfield kujaribu kumburudisha mtu yeyote bali walikwenda kucheza soka.
Mourinho anadai kama kipindi cha pili aliona ugumu kufanya mabadiliko kutokana na Liverpool walivyokuwa wakicheza huku baadhi ya wachezaji wake muhimu akiwemo majeruhi mpya Eric Bailly wakiwa hawamo ndio maana akacheza mchezo huo unaokera kuangalia.
Cha kushangaza zaidi kuhusu Mou na Manchester United yake ni mashuti mawili tu waliyopiga golini kwa Liverpool katika michezo miwili, yaani shuti moja kila mchezo suala linaloonesha ni jinsi gani United wamekuwa wanajilinda tu.
Liverpool hawako katika kiwango kizuri sana na ni wazi kwamba kwa uwezo wa United ilitarajiwa jana wangejaribu kuwasukuma na kucheza mpira lakini wao wakacheza kama wanacheza na Barcelona au Real Madrid.
Mou anaonekana labda ni muoga kufungwa kutokana na alivyoanza msimu kwa mbwembwe lakini pamoja na yote United wamepata alama 1 Anfield inayowaweka nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi Manchester City.

No comments:

Post a Comment