Monday 16 October 2017

Waziri Mkuchika kupeleka ombi Bungeni umri wa kustaafu uongezwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema anakusudia kupeleka ombi maalum Bungeni kuomba umri wa kustaafu kwa Maprofesa uongezwe na kufikia 65 badala ya 55.
Waziri Mkuchika ameyasema hayo alipokwenda alipotembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira na kukutana na watendaji wa taasisi hiyo, na kusema kwamba umri wa kustaafu kwa sheria unawafanya wasomi hao washindwe kutumika vizuri kulijenga Taifa.
"Hawa maprofesa wengi wanaofikia hatua hiyo wanakuwa na miaka kuanzia 50 na kuendelea, halafu anafanya kazi kidogo anatakiwa kustaafu, tutapeleka bungeni maombi kuwe na mabadiliko kidogo katika baadhi ya maeneo, haitakuwa na maana kama wasomi wanatumia rasilimali za taifa kufikia hatua hiyo halafu baada ya kuhitimu wanafanya kazi kwa muda mfupi na kutakiwa kustaafu", amesema Waziri Mkuchika.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuchika ameahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta hiyo, ikiwemo sheria na utaratibu wa ajira unaopitia kwenye Sekretarieti ya ajira.

No comments:

Post a Comment