Friday, 20 October 2017

Mexime asema Kagera Sugar bado inatafuta ushindi

Kocha wa klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Meck Mexime amesema timu yao bado inatafuta ushindi.
Meck ameyasema hayo leo kuelekea mchezo wa raundi ya 7 dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
“Kikubwa sisi tunatafuta ushindi kwasababu hatujaupata tangu ligi ianze, hivyo tumejiandaa kutafuta ushindi na pointi tatu”, amesema Meck Mexime.
Mexime ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya Mtibwa Sugar ameshindwa kuonesha makali ya msimu uliopita tangu ligi ya msimu wa 2017/18 ianze ambapo hajafanikiwa kupata ushindi kwenye mechi Sita za mwanzo.
Hadi sasa Kagera Sugar inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 2. Wakata Miwa hao wa Kaitaba wamepoteza mechi 4 na kutoa sare mechi mbili. Wakati Mwadui wanashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 6 baada ya michezo Sita.

No comments:

Post a Comment