Tuesday, 17 October 2017

Shonza kuanza na wasanii wanaovaa vibaya na kutumia maneno mabaya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza imetangaza kuanza kushughulika na wasanii ambao wanavaa vibaya na kutumia maneno mabaya kwenye kazi zao za sanaa.
Juliana Shonza amesema hayo leo alipokuwa anapokelewa ofisini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe na kusema alipoteuliwa tu aliona kuwa kwenye sanaa hususani wasanii wamekuwa wakivaa vibaya kwenye kazi zao na kutumia maneno yasiyo na maadili kwenye kazi zao hizo na kusema kama serikali lazima wahakikishe wanalifanyia kazi ili kulinda utamaduni wa Tanzania.
"Nilipoteuliwa tu ni jambo ambalo nilianza nalo ni mmomonyoka wa maadili kwa kweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia kwenye nyimbo na kazi za sanaa lugha ambayo inatumika inakuwa siyo nzuri, lakini kama haitoshi kuna nyimbo ambazo zinaibwa ukifuatilia ndani unakuta maadili siyo mazuri, lakini hata katika suala la mavazi mimi nalisema wazi nitawaambia wasanii wa kike wajitahidi kuvaa vizuri, kwa sababu hatuwezi kuacha hivi vitu vikawa vinaendelea tu kila taifa na misingi yake na tamaduni zake" alisema Juliana Shonza
Mbali na hilo Naibu Waziri wa Habari amesisitiza kuwa ni jukumu la viongozi kuhakikisha utamaduni wetu unaendelezwa na kusimamia misingi ya taifa.

No comments:

Post a Comment