Sunday, 14 January 2018

Perez bado ana imani kubwa na Zidane



Klabu tajiri huwa zinawekeza ili kupata makombe tu, hawataki kitu kingine chochote, hawataki kukuza vipaji wala kutafuta nafasi ila kinachotakiwa ni kombe tu na hiyo ndio sera ya Real Madrid.

Jana Real Madrid wametoka kupoteza mchezo wao dhidi ya Villareal, kwa matokeo haya sasa Real Madrid wanabaki na alama 32 na vinara wa ligi Barcelona wakishinda mechi ijayo watawapita Madrid kwa alama 19.

Pamoja na yote hayo lakini sio rahisi kwa Florentino Perez kumfukuza Zinedine Zidane na hawezi kukaa muda mrefu kama Arsene Wenger ama Sir Alex Ferguson lakini kwa siku za karibuni anaonekana hawezi kuondolewa.

Bodi nzima ya Real Madrid ikiongozwa na Rais mwenyewe Florentino Perez pamoja na wachezaji wote wa Real Madrid inasemwa kwamba wako upande wa Zidane na wana imani naye katika timu hiyo.

Habari kutoka Hispania zinasema kwamba Florentino Perez anajipanga kutoa fungu kubwa la pesa kwa Zinedine Zidane kwa ajili ya usajili wa mwezi huu wa January na lile dirisha kubwa la usajili baada ya msimu wa ligi.

Zidane anaweza kuendelea kupewa nafasi na imani katika kikosi cha Real Madrid lakini yeye mwenyewe kama asiporidhishwa na kiwango cha klabu hiyo anaweza kuamua kuachana nayo kwa hiari yake.

No comments:

Post a Comment