Michael Olunga amekuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi kuu ya Uhispania ~La Liga. Olunga amefunga magoli matatu (Hat-trick) dhidi ya Las Palmas na kuweka rekodi ya kuwa Mkenya wa Kwanza kufunga hat-trick kwenye Laliga.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kuona taarifa hiyo hakukaa kimya kupitkia ukurasa wake wa Facebook akampongeza Michael Olunga kwa kusema “Ongera Michael Olunga kwa kuweka historia kuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi ya Hispania La Liga na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwa klabu ya Girona katika ligi ya Spain”
Nae kiongozi wa Muungano wa Upinzania nchini Kenya Raila Odinga amepost katika ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Olunga.
No comments:
Post a Comment