Suzan Michael ‘Pretty Kindy’.
MSANII wa filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kindy’ ambaye siku chache zilizopita alipewa kibano cha kufungiwa asifanye sanaa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza, amesema kuwa jambo hilo limempa funzo kubwa na kuamua kubadilika kimavazi.
Akizungumza na paparazi wetu, Pretty alisema tangu naibu waziri ampe adhabu hiyo kwa kosa la kuweka picha ya utupu mtandaoni, amekuwa akiwaza mengi na kuona kuna haja ya kuufyata kwa kubadili mfumo wa mavazi yake, sababu amegundua mavazi ya utupu yanamshushia heshima.
“Kwa upande mwingine kanipa funzo kubwa maishani mwangu, tangu ile adhabu itokee, hata ukikutana na mimi utagundua hiki ninachokisema, nimebadilika mno kimavazi, navaa kiheshima, nimegundua nguo za nusu utupu zinanifanya nidharaulike tu,” alisema.
No comments:
Post a Comment