Thursday, 7 December 2017

Kitendo cha Trump kuutambua Jerusalem kuwa mji mku wa Israel,Saudi Arabia walaani hatua hiyo


Donald Trump

Saudi Arabia imelaani hatua ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel huku pia shutuma zikizidi kuongezeka kufuatia hatua hiyo.

Katika taarifa, taifa hilo la ghuba lilisema kuwa tangazo hilo la Trump sio la haki.

Lakini waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alilitaja tangazo hilo kuwa la kihistoria.

Hatma ya mji wa Jerusalem ni moja masuala makuu kwenye mzozo katika ya Israel na Palestina.

Mataifa 8 kati ya 15 ambayo kwa sasa ni wanachama wa baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa yametaka shirika hilo kufanya mkutano wa dharura kufuatia uamuzi huo wa Marekani.

Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni jambo ambalo halijatambuliwa kimataifa na hadi sasa nchi zote zimeweka balozi zao kweny mji wa Tel Aviv.

Jerusalem una semue takatifu kwa dini tatu za kiyahudi, kiislamu na kikristo.

Wapalestina walichoma picha za Trump



No comments:

Post a Comment