Friday 8 December 2017

Askari Mgambo Kizuizini kwa kujifanya Maofisa Uhamiaji



Mwanza. Idara ya uhamiaji jijini Mwanza inawashikilia kwa mahojiano askari mgambo wawili wa jiji la Mwanza kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa idara hiyo na kupita maeneo ya biashara ikiwemo mahoteli kukagua vibali vya ukaazi wa wageni.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Paul Eranga akitoa taarifa leo Ijumaa amesema mgambo hao walikamatwa walipofika kwenye moja ya hoteli za kitalii jijini Mwanza kwa lengo la kukagua wageni waliofikia hapo iwapo wana nyaraka na vibali halali vya kuingia nchini.

Amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Chacha Kichele, mkazi wa Bugarika Wilaya ya Nyamagana na mwenzake Michael Julius, mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela.

“Walitumia mwanya wa sare zao kufanana na zile za idara ya Uhamiaji kupita kwenye mahoteli kukagua wageni wakijifanya ni maofisa Uhamiaji hadi uongozi wa hoteli moja ulipowashtukia na kutoa taarifa,” amesema Eranga

No comments:

Post a Comment