Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla jana Desemba 8,2017 Mjini Dodoma, ameunda kamati ya kuongoza maandalizi ya namna watanzania na wageni wa Tanzania watakavyosherehekea Utanzania wao kwenye mwezi maalum utakaojulikana kama ‘TANZANIA HERITAGE MONTH’.
Akielezea wakati wa kutangaza kamati hiyo iliyojumlisha wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari, wanamichezo na wadau wengine mbalimbali na wafanyabishara, alisema:
“Kwenye mwezi huu kila kitu kitakuwa cha kitanzania na tutataka kwenye kila ofisi ya umma, ofisi binafsi, shule, chuo, hotel, balozi zetu n.k mtu akifika tu, ‘utanzania’ wetu uonekane!” alieleza Dk.Kigwangalla.
Utanzania huo ambapo kila mwezi huo utakapofika ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na aina ya mavazi maalum, vyakula, na mambo mengine yanayobeba na kujumuisha Utanzania.
No comments:
Post a Comment