Thursday, 7 December 2017

Kitendo cha Faiza kujianika utupu akiwa leba, Wolper ampa tano


Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amesema kuwa, anamuunga mkono muigizaji Faiza Ally kwa kitendo chake cha kuweka picha inayomuonyesha akiwa mtupu katika chumba cha kujifungulia (leba).

Wolper alisema anawashangaa watu wanaomponda Faiza aliyeposti picha hiyo hivi karibuni katika ukurasa wake wa Instagram, wakati yeye amevutiwa sana na kitendo hicho na ipo siku atamuiga.

“Wabongo ni washamba, ushamba unawasumbua sio kingine. Sioni ubaya wa hiyo picha hata kidogo, eti katudhalilisha, kamdhalilisha nani sasa pale, mimi nimefurahi mno tena nitamuiga nikijaaliwa kupata mtoto,”alisema Wolper.



No comments:

Post a Comment