Friday, 8 December 2017

Watu wawili waliokutwa na Mayai ya Mbuni wahukumiwa miaka 25 Jela



Serengeti. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya  Serengeti imewahukumu kifungo cha miaka 25 washitakiwa wawili na gari lao kutaifishwa kwa kosa la kukutwa na mayai 16 ya mbuni yenye thamani ya zaidi ya Sh 42 milioni.

Waliokumbwa na adhabu hiyo ni Marwa Matiko(32) na Julius Marwa (42) wakazi Tarime mjini.

Akitoa hukumu leo Ijumaa katika kesi ya uhujumu uchumi namba 128/2016 hakimu wa mahakama hiyo, Ismael  Ngaile amesema kila mshitakiwa atahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela na gari lao kutaifishwa liuzwe.

Mapema mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Emmanuel Zumba ameiambia Mahakama kuwa, washitakiwa hao walikamatwa Desemba 7, 2016 wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni Serengeti wakiwa na mayai 16 ya mbuni yenye thamani ya zaidi ya Sh 42 milioni kinyume cha sheria.

Amesema mayai hayo walikuwa wameyaficha ndani ya gari lao.

Amesema washitakiwa wakidai kuwa walikuwa wanapeleka nchini Kenya kwa ajili ya kuuza kwa watu wanaotengeneza dawa ya ukimwi.

No comments:

Post a Comment