New York, Marekani. Kampuni ya Google inayomiliki mtandao wa kurusha video wa Youtube imeanza kuajiri watu wa kupitia video na kuondoa zilizo kinyume cha maadili.
Mtandao huo pia umeanzisha kanuni kali zitakazosaidia kuondokana na kadhia ya video zinazokinzana na maadili.
Hadi mwakani, kampuni hiyo imepanga kuajiri watu 10,000. Mkurugenzi wa Youtube, Susan Wojcicki amesema wataajiri watu wengi zaidi Desemba na Januari,2018.
Amesema wanalazimika kufanya hivyo kwa sababu katika kipindi cha miezi sita wameshuhudia video zaidi ya 2 milioni zilizokuwa zikichochea uhalifu na nyingine za ugaidi.
"Tutafuatilia maoni yanayotolewa na watazamaji pia, tutayaondoa iwapo yatabainika yana nia ovu ya kushambulia au kuchochea uhalifu,” amesema Susan.
Mtandao wa Youtube uliingia matatani hivi karibuni baada ya kudaiwa kuwapo video za udhalilishaji watoto. Kampuni nyingi kubwa duniani zilijiondoa kutangaza katika mtandao huo.
No comments:
Post a Comment