Sunday, 17 December 2017

Dk Mwakyembe Awapongeza Sportpesa Kudhamini Tusa, Ataka Wengine Wawaige



Waziri wa Michezo Dk Harrison Mwakyembe amewapongeza Sportpesa lianza kwa kushukuru SportPesa kwa kudhamini mashindano hayo ya Vyuo Vikuu (TUSA) yanayoendelea mjini Dodoma na kuomba kampuni mengi kuiga mfano wa kampuni hiyo.
Dk Mwakyembe amesema udhamini wa makampuni umekuwa msaada mkubwa katika kusaidia kuendeleza michezo katika nchi mbalimbali.
“Kuna wachezaji au makocha wengi wametokana na michezo ya vyuoni sote tunajua, sasa anayedhamini michezo vyuoni anajua faida yake kuwa ni ya baadaye lakini kubwa kwa taifa, hivyo niwapongeze hawa SportPesa kwa kazi nzuri,” alisema.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo Ofisa Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya alisema yafuatayo:
"Sisi kama SportPesa, tukiwa wadau wa maendeleo ya michezo nchini, hatukuwa na kigugumizi tulipoombwa kuyadhamini mashindano haya ya vyuo vikuu kwa maana moja kubwa,
Hakuna asiyejua jinsi vipaji vingi vya michezo na Sanaa vinavyopatikana kutoka kwa wanafunzi wa sekondari wa nyuo vikuu, nah ii ni duniani kote.
Ni kwasababu hiyo, nchi kama Marekani inajivunia kuwa na ligi ya mpira wa kikapu ya NBA iliyosheheni nyota wakubwa kama vile Kevin Durant na Stephen Curry ambao wametoka vyuoni na kuingia kwenye ligi moja kwa moja.
Kupitia mfano huo, imefika kipindi tunatakiwa kujua kuwa wasomi wetu si tu kwamba wamejaliwa uwezo wa kupambana na madesa, lakini pia wana vipaji vikubwa katika sanaa na michezo na ndio maana sitashangaa kusikia mtu kama Didier Drogba ni mhasibu wa ngazi ya Chuo Kikuu bila kumsahau mzee Arsene Wenger mwenye degree ya uchumi.
Nimalize kwa kuwapongeza nyote mliopo hapa hususani wachezaji kwani tunajua mmeacha madesa vyuoni na mkirudi mtakuta assignment za kutosha bila kusahau test one ambazo ndio msimu wake huu.
Tunaamini sio tu kwamba mtakuja kulitumikia taifa kama wasomi wa taaluma mbalimbali, lakini pia katika tasnia ya michezo kwani hapa hamkuja kwasababu ya GPA zenu bali ni vipaji vyenu.

No comments:

Post a Comment