Friday, 8 December 2017






Mwanza. Sakata la mwanamke aliyemvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwatia mbaroni watu wengine watatu akiwemo aliyevishwa pete.
Sura mpya ya kwanza ni mtuhumiwa Milembe Suleiman (36), anayedaiwa kumvalisha pete mwanamke mwenzake Janeth Shonza, aliyekuwa akishikiliwa na polisi mkoani Geita kuhamishiwa mkoani Mwanza.
Pili, jeshi la polisi pia limefanikiwa kumtia mbaroni mwanamke aliyevishwa pete, Janeth Shonza (25), mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa mafichoni eneo la Puma mkoani Singida.
Amewataja wengine wanaoshikiliwa na kutarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika kuwa ni Richard Fabian (28), mkazi wa Buzuruga jijini Mwanza aliyepiga na kusambaza mitandaoni picha za wanawake hao wakivishana pete mitandaoni.
Kamanda Msangi amemtaja mwingine anayeshikiliwa kuwa ni Aneth Mkuki (24), mkazi wa Nyasaka jijini Mwanza, mpenzi mwingine wa Janeth aliyemsaidia kutoroka kukwepa kutiwa mbaroni na polisi baada ya video yao kusambazwa mitandaoni.

No comments:

Post a Comment