Saturday, 9 December 2017

Lwandamina agoma wachezaji vijana kutolewa kwa mkopo



ocha George Lwandamina ameonekana kuwa na imani kubwa na wachezaji vijana wa kikosi hicho.

Lwandamina âmezuia kuondoka kwa wachezaji wote vijana walio katika kikosi chake hasa wale waliokuwa wakiombwa kwa mkopo.

Kocha huyo raia wa Zambia, ameuisisitiza uongozi wa Yanga wachezaji wa Yanga walio katika kikosi hicho wanapaswa kuendelea kubaki.

“Kocha amekataa kabisa wachezaji vijana wasiondoke, amesisitiza waendelee kubaki hadi hapo baadaye kwa kuwa ana programu nao,” kilieleza chanzo.

Timu kadhaa, zilionekana kuanza kuwanyemelea wachezaji makinda wa Yanga katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lakini Lwandamina ameonekana kuendelea kuwahitaji.

Lwandamina amekuwa ni muumini wa vijana na tokea ametua Yanga amekuwa akitoa nafasi kwa wachezaji vijana ambao wamekuwa wakionekana kufanya vema.

No comments:

Post a Comment