Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry ameliagiza Jeshi la polisi mkoani humo kumsaka na kumtia nguvuni mwanaume mmoja mkazi wa wilaya ya Urambo anaedaiwa kupanga njama za kumuua mke wake kwa kutumia jambazi ambae hakuweza kutimiza jukumu hilo.
RC Mwanry ametoa agizo hilo katika kilele cha kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizofanyika katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo zilizoandaliwa na kituo kimoja cha redio mkoani humo.
Kituo hicho baada ya kuandaa kampeni hiyo kilirekodi mkasa wa huyo mama aliofanyiwa na mumewe na kukiweka kipande hicho cha sauti kwenye redio. Huku mama huyo hakutakiwa kuonekana kwasababu za usalama wake.
Kufuatia kusikika kwa mama huyo redioni ndipo RC huyo akatoa maagizo kwa jeshi la polisi kumsaka popote alipo.
No comments:
Post a Comment