Polisi siku ya Jumatano walimkamata mgonjwa aliyemuua nesi kwa kumpiga risasi ya kichwa kwenye kituo cha afya cha Chiromo huko Westlands, Nairobi
Mgonjwa huyo aliyetambuliwa kwa jina la Joseph Njoroge Mungai mwenye kibali cha kumiliki silaha alimpiga risasi ya kichwa daktari huyo aliyefahamika kwa jina la Faustine Mwandime Mwandilu
Kamanda wa polisi wa Nairobi Japheth Koome amesema mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kwa kesi ya mauaji
Mtuhumiwa huyo mwenye matatizo ya akili alipelekwa na kulazwa hospitalini hapo akiwa na bunduki baada ya kukataa kuiwasilisha kwa walinzi wa hospitali
No comments:
Post a Comment