Wednesday, 31 January 2018

Karia kuongoza ujumbe wa TFF mkutano wa CAF


Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limetoa taarifa leo kuwa viongozi wake watatu wa juu watakuwa ni miongoni mwa wajumbe watakaohudhuria mkutano mkuu wa CAF.

Viongozi hao ni Rais wa TFF Wallace Karia, Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred.

Mkutano huo mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF utafanyika Februari 2, 2018 nchini Morocco.

Morocco ni mwenyeji wa michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN zilizoanza Januari 13 na leo ni hatua ya nusu fainali ambapo wenyeji Morocoo wanacheza na Libya huku Sudan wakikipiga na Nigeria.

Shule iliyoongoza kidato cha nne yataja siri ya ufaulu


Baada ya shule ya Sekondari ya wasichana ya St. Francis Mjini Mbeya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana wameeleza kuwa bidii ya walimu na wanafunzi ndio siri ya mafanikio hayo.

Wakizungumza na EATV  baadhi ya walimu akiwemo Mwalimu wa Somo la Kemia ambaye pia ni Mwalimu wa Nidhamu katika Shule hiyo, Neema Kimani, Mwalimu Msaidizi wa Taaluma Reginald Chiwangu bidii na kumtanguliza Mungu ndio siri ya mafanikio hayo.

''Kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, bidii ya walimu na wanafunzi, utawala bora na kusikiliza ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu ndio vimechangia shule yetu kuongoza kitaifa'', wamesema.

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo akiwemo Joyce Msigala, Lorette Leone na Bibiana Karumuna wamesema kuwa matokeo hayo yametoa mwanga wa jinsi gani  walijiandaa ili kufanya vizuri kwenye mtihani wao.

Wahitimu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya St. Francis waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ambao ndio wameongoza kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza walikuwa 92.

EATV.

Nape aipongeza Serikali kuhusu umeme na kuipa ushauri


Mbunge Nape Nnauye leo Bungeni ameipa changamoto Serikali juu ya gharama za kuunganisha umeme na kuishauri kuendelea kuchaji elfu 27,000 hata baada ya mradi REA kupita ambapo wataanza kuchaji 177,000 kuunganisha umeme.

Nape Nnauye ametoa ushauri huo alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwenda kwenye Wizara ya Nishati

"Kwanza niipongeze Serikali chini ya Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri wanayofanya ya usambazaji mzuri wa umeme vijijini hasa REA awamu ya 3, kwa kuwa gharama za kuunganisha umeme wakati mradi unaendelea ni elfu 27,000 na mradi ukipita ni 177,000 na kwa kuwa idadi kubwa na nzuri ya watumiaji wa umeme ni biashara nzuri kwa TANESCO kwanini bei hii isiwe moja ya elfu 27" alisema Nape Nnauye

Hata hivyo Nape Nnauye aliendelea kusisitiza kuwa kama jambo hilo halitawezekana basi REA waendelee na uwekaji wa nguzo na miundombinu na TANESCO wafanye kazi moja ya kupeleka umeme na kukusanya kodi baada ya kupeleka umeme.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati alijibu hoja hiyo na kudai kuwa amepokea ushauri huo wa Mbunge wa Mtama na kuwa atapeleka katika ngazi zingine na kuona Serikali nini itafanya

"Wazo alilosema Kaka yangu Nape Nnauye linapokelewa na litafanyiwa kazi kwani ni la msingi kwa sababu Wizara yetu na shirika letu la TANESCO na wadau wengine wa nishati tunauza bidhaa hii hivyo ni vema tunapouza tupate wateja wengi ili tupate mapato na kuendesha shughuli mbalimbali na uwekezaji mpya wa maeneoya nishati"

Mbunge aliyesimamia kuapishwa kwa Odinga atiwa mbaroni


Jeshi la Polisi nchini Kenya, leo Januari 31, 2018 mchana limemtia mbaroni mbunge wa Jimbo la Ruaraka, Tom J Kajwang’, ambaye alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park jana Jumanne.

Kajwang amekamatwa na maofisa hao waliokuwa wamevalia kiraia nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho nchini humo.

Kajwang’ na mwanasheria mwingine Miguna Miguna, ndiyo walisimamia matukio yote ya “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa watu’ katika viwanja vya Uhuru Park. Imeelezwa kuwa, Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi ambapo alish

Wasanii wa filamu watoa msaada wa vifaa tiba

Wasanii wa filamu kutoka taasisi ya ‘Binti Filamu Foundation’ yenye wanawake kumi wa kundi la waigizaji la Bongo Muvi, leo wametoa msaada wa vifaa-tiba vyenye thamani ya Sh. Mil. 30 katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, mmoja wa wasanii hao, Halima Yahya ‘Davina’ alisema:
“Tumejipanga kuwafikia wanawake na mabinti wengi zaidi ili kutoa elimu ya ujasiriamali, kuwaeleza jinsi ya kukabiliana na masuala ya ukatili kwa wanawake na tutajikita zaidi kwenye afya kwani tunaaamini malengo hayo hayawezi kutimia bila afya bora.

“Hivyo tumeamua kuanza na kampeni rasmi katika hospitali tukihamasisha wadau, makampuni na wananchi kwa ujumla kuwekeza katika afya, kuunga mkono juhudi za serikali za awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli yenye kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

“Binti Filamu Foundation kwa udhamini mkubwa wa Scientific Suppliers pia tumetoa vifaa-tiba vyenye thamani ya Sh. milioni 30 kuunga mkono juhudi za serikali kujali afya ya mama na mtoto.”

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Wilaya ya Kinondoni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Benjamin Sitta, amesema wasanii wanapaswa kuwa nguzo kubwa katika jamii na wanasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo nchini. Akaongeza kuwa wasanii wengi wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo, Mganga Mkuu Mfawidhi katika hospital hiyo, Isdory Kiwale, amesema wanashukuru msaada huo huku akiwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitatumika kama vilivyo kusudiwa.

Malengo makuu ya taasisi hiyo ni kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na raia wengine kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni, mauaji ya albino na vikongwe na mengine yananyolenga kudhalilisha utu wa mwanadamu.


Meya Sitta Apokea Msaada Wa Vifaa Tiba Vyenye Thamani Ya Milioni 30



Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amepokea vifaa tiba vitakavyotumika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam vyenye thamani ya Shilingi milioni 30 kutoka kwa taasisi ya Binti Filamu Foundation ambayo inaundwa na wasanii kumi wa filamu nchini Tanzania.

Meya Sitta ameishukuru taasisi hiyo kwa kutoa vifaa hivyo ikiwa ni lengo la kusaidia jamii kukabiliana na changamoto zinazoikumba sekta ya afya  hususani mama na mtoto ambao ni wahitaji wakubwa wa misaada hiyo.
"Ninafurahi na naawapongeza Binti Filamu Foundation kwa kutoa msaada huu na iwe chachu kwa wasanii wengine kuiga mfano kama wenu kwa kusaidia jamii yenye mahitaji kuliko kila siku kuigwa na kuandikwa mabaya, lazima mtumie akili zenu ili watu waige yaliyo  mazuri, amesema Meya sitta.

Kwa upande wake mlezi na mshauri wa Taasisi hiyo Bi, Asha Baraka amesema kuwa lengo ni kusaidia watoto, kinamama na baadae wazee ili kuunga jitithada za Mama Janeth Magufulli ambae anasaidia wazee na kina mama ambao hawana uwezo.


Nae Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala Dr. Isdory Kiwale ameishukuru taasisi hiyo kwani siyo mara ya kwanza kufika hospitalini hapo na kutoa msaada walishanya hivyo kipindi ilipohitajika damu ili kuokoa maisha ya watu, walijitolea kutoa damu.

Akisoma risala mbele ya mgeni Halima Yahaya amesema kuwa Binti Filamu Foundation imefikia kina mama zaidi  ya elfu 7 Tanzania bara na visiwani  huku wakitoa elimu kupinga unyanyasaji wa kijinsia ambao upo kwenye jamii ya Kitanzania.

 Aidha kupitia mpango huu tunashirikiana na taasisi mbalimbali za wanawake  kama vile jukwaa la wanawake  ambapo huendesha kampeni ijulikanayo kama ''ELIMIKA NA BINTI FILAMU'' mwaka 2016/2017 na mwaka huu kauli mbiu ni ''Silaha ya mwanamke ni malengo'' ikiwa lengo na la kuwafikia wanawake zaidi ili kuwaelimisha kuhusiana na unyanyasaji na pia kusaidia sekta ya afya  kwani malengo hayawezi kufikiwa bila kuwa na afya bora.



Tuesday, 30 January 2018

VIDEO: Rosa Ree akana Bifu na Navy Kenzo, Chemical

RAPA anaefanya vizuri kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Rosa Ree amekana kuwa na bifu na wakali Navy Kenzo, Chemical. Rosa Ree ameyasema hayo alipokuwa akitambulisha ngoma yake mpya kwa mara ya kwanza ndani ya Muungwana TV inayoitwa Marathoni ambayo amempa shavu hitmaker wa Sina Jambo, Bill Nas


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI .............USISAHAU KUSUBSCRIBE..............

Mshindi wa pili kidato cha nne amtaja Mungu na wazazi wake


Elizabeth Mangu, mshindi wa pili Kitaifa katika mitihani ya kidato cha nne  amesema kumtanguliza Mungu katika kila kitu  ndoto ya kuwa wa kwanza, bidii kwenye masomo na usimamizi wa karibu wa wazazi na walimu ndiyo  siri ya mafanikio yake.

Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Mwanza leo Januari 30, Elizabeth amesema  tangu alipojiunga kidato cha kwanza, alijiwekea lengo la kushika nafasi ya kwanza katika mitihani ya Taifa na aliwafuata walimu wake kuomba ushauri wa kufanikisha lengo hilo.

“Niliweka lengo la kushika nafasi ya kwanza kama alivyofanya Robina aliyeongoza mitihani ya kitaifa akitokea shule yetu ya Marian Girls; nilimfuata Mwalimu wa taaluma Ihonde na mwenzake wa Civics anayeitwa Mwanduzi kuwaomba ushauri wa kufanikisha hilo,” anasema na kuongeza

“Wote walinishauri kuzingatia masomo, kusoma pamoja na kusaidia wenzangu darasani kama njia ya kujifunza, kuzingatia maelekezo ya walimu na wazazi shuleni na nyumbani pamoja na kumcha Mungu kama mwanzo wa hekima,”

Akizungumza mbele ya mama yake mzazi, Wande Mandalu ambaye ni mwalimu katika shule ya Sekondari ya Kiloleli jijini Mwanza, Elizabeth alisema mwongozo na ukali wa wazazi wake aliposhuka kitaaluma pia imesaidia mafanikio yake.

“Nawashauri wazazi wawe karibu na kufuatilia mienendo ya watoto wao kuanzia nyumbani hadi shuleni na kuwatia moyo wanapofanya vema bila kuacha kuwaonya na kuwakaripia wanapokosea,” amesema

Kauli hiyo iliungwa mkono na mama yake, Wande Mandalu pamoja na Mwalimu wake wa masomo ya dini katika Kanisa la KVCC, Geofrey Lugwisha waliosema liha ya kuwajenga watoto katika imani ya kiroho, wazazi wana wajibu wa kuwasaidia watoto wao kielimu, kuwapongeza na kuwaonya wanapopotoka.

“Wazazi lazima tuwe wasimamizi wa karibu kwa kufuatilia nyendo za watoto kuanzia nyumbani, shuleni hadi mitaani; lazima wajua ratiba na kuwapa miongozo inayofaa maishani, hasa msisitizo kwenye elimu ambayo ndio urithi wa kudumu,” amesema  Mwalimu Mandalu, mama wa watoto watatu

Eliza ni mtoto wa pili katika familia yake ya watoto watatu akitanguliwa na kaka yake Joseph Mangu na mdogo wake, Carren Mangu aliyesoma kidato cha kwanza shule ya wasichana ya Marian.

Mashabiki wa Arsenal wamuona Aubameyang kama Henry mpya


Mashabiki wa Arsenal tayari wamenunua jezi ya Pierre-Emerick Aubameyang yenye namba 14, wakati nyota huyo wa Dortmund akiwa njiani kwenda Emirates.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wameonekana wakiwa wamevaa jezi ya mshambuliaji huyo wa Dortmund ikiwa na jina lake namba 14, namba hiyo ilikuwa kivaliwa na mshambuliaji Thierry Henry na Theo Walcott.

Gunners sasa inakimbizana na muda katika kukamilisha utakaovunja rekodi wa pauni 55.4milioni kwa nyota huyo wa Gabon (28).

Hiyo itampa nafasi Aubameyang kuungana na nyota mwenzake wa zamani wa Dortmund Henrikh Mkhitaryan alijiunga na Arsenal akitokea na Manchester United kwa kubadilishana na Alexis Sanchez wiki iliyopita.

Ujio wa Aubameyang unamweka katika wakati mgumu mshambuliaji Alexandre Lacazette aliyesajiliwa mwanzo wa msimu huu kwa pauni 46.5milioni akitokea Lyon.

Hata hivyo uamuzi wa shabiki kupiga picha akiwa na jezi ya Aubameyang umepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wengine wa Emirates.

Taarifa zinasema kuwa Arsenal wamekubali kununua nyota huyo ambaye anatagemewa kuaga Borussia Dortmund ndani ya saa 24 zijazo.

Shabiki mmoja alitweeted: Love you Aubameyang." Lakini wenzake wakamjibu "Acha kwanza asaini."

Straika wa Uganda aitamani VPL


Straika Hood Mayanja, anayekipiga katika klabu ya African Lyon, inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza, amesema anajitahidi kufanya vizuri ili timu iweze kurudi Ligi Kuu.

Mayanja aliondoka nchini na baadaye kurudishwa kwa kazi moja tu, kuifanya timu hiyo irudi juu sasa isiporudi atakuwa ajatimiza ndoto yake.

"Niliitwa kwa kazi moja tu kuhakikisha kwamba timu inarejea Ligi Kuu, mimi nilikuwa muda mrefu hapa nikaona nirudi nije kupambana iweze kufanya vizuri turejee juu, lakini natakiwa kushirikiana na wenzangu ili tuweze kusogea," alisema.

Aliongeza kwamba, kadri miaka inavyozidi kwenda ndio ligi daraja hilo linazidi kuwa ngumu, hivyo kama wakifanikiwa kupanda, hawatoleta mzaha tena.

"Miaka inavyozidi kwenda ndio ugumu wa ligi unazidi kuonekana yaani, sasa kama tukifanikiwa kupanda hatutoleta masihara badala yake tutahakikisha kwamba tunasalia katika ligi," alisema.

Mayanja aliondoka klabuni hapo msimu uliopita, wakati timu hiyo ikiwa inashiriki Ligi Kuu na kujiunga na Mbeya City, lakini alijikuta na wakati mgumu badala yake akatimkia kwao Uganda, lakini amerejea tena nchini na anapambana kuirudisha upya timu hiyo katika Ligi.

Wachimbaji wanne wa mchanga wafariki Arusha



Watu wanne wamefariki dunia huku mmoja akijeruhiwa vibaya baada ya mawe kuporomoka na kuwafukia wachimbaji  watano ambao walikuwa wakichimba mchanga kwenye eneo la mlima CCM Kata ya Muriet, Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Charles Mkumbo akiongea na www.eatv.tv amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kudai kuwa majeruhi amepelekwa katika hospitali ya Mount Meru huku hali yake ikiwa ni mbaya sana.

"Kuna eneo lipo huku Kata ya Muriet ambapo huwa wanachimba mchanga mkavu hivyo wakati wanaendelea na kuchimba kuna sehemu nyingine huwa haichimbwi sasa wanasayansi wanatuambia dunia huwa inazunguka hivyo kuna mpasuko ulikuwa umetokea kwenye eneo ambalo wala halichimbwi huo mchanga, hivyo hilo gema lilipopasuka likaangukia upande ambao watu wanachimba mchanga huo na kuwafukia watu watano, wanne walipoteza maisha pale pale huku mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu" alisema Mkumbo.

EATV

Rostand aiokoa Yanga na aibu kombe la FA


Kipa Youthe Rostand ameibuka shujaa baada ya kupangua penalti 3 na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

Yanga ilikuwa ikiivaa Ihefu katika mechi ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo.

Kipa huyo wa Cameroon amepangua mikwaju mitatu ya penalti wakati wa changamoto za mikwaju hiyo.

Al manusura Yanga ing’olewe baada ya Obrey Chirwa kukosa penalti, lakini kipa huyo Mcameroon akapangua penalti iliyofuata na kuifanya Yanga iendelee.

Yanga ililazimika kuingia kwenye changamoto hizo na timu hiyo ya daraja la pili baada ya kusawazisha katika dakika za majeruhi baada ya kuwa imefungwa bao.

Chirwa ndiye aliyesawazisha kwa mkwaju wa penalti huku Ihefu wakiwa wanaamini mechi ilikuwa imeisha.

'Kama Mollel atashinda Serikali itatatua tatizo la Kilelepori'


Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeahidi kumuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba na Waziri wa Ardhi   William Lukuvi, kufika Siha kutatua tatizo la Kilelepori na wananchi wanaozunguka eneo hilo, endapo Dk. Godwin Mollel atashinda.

Akimnadi Dk.Mollel, katika kata ya Donyomurwak, Katibu wa itikadi na uenezi CCM Taifa, Humphrey Polepole, amesema  eneo la Kilelepori ni mali ya Siha, hivyo Chama hicho kikishinda, Serikali itafika ili kuona namna ya kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wananchi na  eneo hilo la Kilelepori ambalo limekuwa likitumiwa na shule ya Taaluma ya Polisi Moshi (MPA) kwa mazoezi ya kijeshi.

"Natambua mnakabiliwa na changamoto kubwa na eneo la kilelepori, na hii ni kutokana na wananchi kuendelea kuongezeka na mji kupanuka sasa nipeni Dk.Mollel ili Serikali iweze kushirikiana naye kutatua changamoto hii ambayo inawasumbua muda mrefu" amesema  polepole.

Polepole amesema  siasa za matukio na uongo zimepitwa na wakati hivyo ni vyema wananchi wakatambua Serikali ya chama cha mapinduzi ina dhamira ya dhati ya kuwasaidia na kutatua changamoto zote zinazowakabili.

Akiomba kura Dk.Mollel aliwaomba wananchi wamchague ili aweze kushughulikia tatizo la maabara kwa shule za kata na kuhakikisha zinakuwa na vifaa ili kuwezesha masomo ya sayansi kusomwa kwa vitendo.

Mollel  amesema  pia atashughulikia tatizo la maji na kuhakikisha wananchi wa kata ya Donyomurwak wanasambaziwa huduma ya maji safi na salama kwa matumizi ya kunywa, pamoja na kushughulikia tatizo la umeme na migogoro ya Ardhi.

 Akiomba kura Mgombea udiwani wa Kata ya Donyomurwak, Lwite Ndosi, ambaye hivi karibuni alijiondoa Chadema na kugombea tena nafasi hiyo kupitia chama Tawala, amewaomba  wananchi wamchague tena ili kuweza kushughulika na changamoto zao ambazo ni miundombinu ya barabara, ujenzi wa Bweni la wasichana shule ya Sekondari Sikilari pamoja na ujenzi wa zahanati katika vijiji vilivyopo katika Kata hiyo.

Ndosi ambaye anachuana vikali na aliyekuwa meneja kampeni wake 2015,Sione Mollel (Chadema)alisema akipewa nafasi hiyo, pia atashughulikia mgogoro uliopo baina ya wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka kambi ya Jeshi (Kilelepori) pamoja na kutoa elimu ya mpango mji kijiji cha Munge ambacho kinakua kwa kasi.

"Nimerudi kwa nguvu na kasi mpya, sasa naomba nipeni tena nafasi hii ili niweze kushughulika na changamoto zenu, naahidi pia nitasaidia wananchi ambao wanalalamika maeneo yao kuchukuliwa na Kulelepori ambao ni wa vijiji vya Munge, Emboko, Loiwa na Ormelili"amesema

Akiomba kura mgombea ubunge jimbo la Cuf,Tumsifuel Mwanri, aliwataka wananchi wa Siha kumchagua, kumchagua, kwa kuwa yeye ana msimamo na anaweza kukaa bungeni kuwatumikia wananchi kwa kipindi chote bila kujiuzulu.

Mwanri amesema  katika uchaguzi huo mdogo wapo wagombea Wanne wa vyama tofauti Siha, lakini ni jukumu la wananchi wa Jimbo hilo wakachukua maamuzi sahihi ya kumchagua Mgombea wa Cuf ambaye atawatumikia kwa uaminifu.

"Ndugu wananchi, angalieni kiongozi ambaye atawatumikia kwa uaminifu, kwani mkimchagua mwingine anaweza kukaa tena mwaka mmoja na kujiuzulu na kuturudisha tena kwenye uchaguzi" amesema

Mwanri amesema  endapo atashinda, pia atashughulikia tatizo la maji na kuhakikisha, gharama zinashuka tofauti na ilivyo sasa ambapo inakuwa mzigo mkubwa kwa wananchi.

Aidha amesema  Siha ina  ardhi nzuri yenye rutuba lakini haitumiki ipasavyo, hivyo akichaguliwa atashughulika na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kushughulikia tatizo la migogoro na kulipatia ufumbuzi.