STAA mpya wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang jana alianza mchezo wake wa kwanza kwenye timu hiyo na kufanikiwa kuifungia bao moja kwenye ushindi wa 5-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Aubameyang amejiunga na Arsenal kwenye dirisha hili la usajili na huu ulikuwa mchezo wake wa kwanza kuitumikia timu hiyo ya London na kupata ushindi mnono hata hivyo Aaron Ramsey aligeuka nyota kwenye timu hiyo baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’.
Arsenal ilianza mchezo huo kwa kasi ya hali ya juu na ndani ya dakika 20 za kwanza timu hiyo ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Ramsey, alifanikiwa kuifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya sita ya mchezo akimalizia pasi safi ya Henrikh Mkhitaryan, ambaye alipata pasi kutoka kwa Mesut Ozil.
Dakika ya 14, Laurent Koscielny, alifanya kazi kubwa baada ya kuifungia Arsenal bao la pili baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Shkrodan Mustafi.
Iliwachukua Arsenal dakika sita tu kujipatia bao la tatu ambalo liliwekwa tena kimiani na Ramsey na kuwafanya waendelee kutakata.
Dakika ya 36 ya mchezo, Mkhitaryan alifanya kazi kubwa na kutoa pasi yake ya pili ya bao baada ya kumtengea Aubameyang mpira safi ambaye hakufanya kosa na kuuchopu akaifungia timu yake bao la nne.
Hata hivyo, Theo Walcott ambaye anaitumikia Everton akiwa anacheza mchezo wake dhidi ya timu yake ya zamani alionyesha kiwango kizuri kipindi cha kwanza ambapo alitolewa uwanjani katika dakika ya 63 na kupigiwa makofi na wachezaji pamoja na mashabiki wa timu hiyo ya London kuonyesha heshima kwake.
Dakika mbili baada ya kutolewa Everton walifanikiwa kujipatia bao moja kupitia kwa Calvert Lewin na kufanya matokeo kuwa 4-1.
Kipa wa Arsenal, Petr Cech aliumia na kutolewa kwenye mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na David Ospina katika dakika ya 69.
Dakika ya 74, Ramsey alikamilisha `hat trick’ yake baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Mkhitaryan ambaye naye alitoa pasi ya tatu ya bao kwenye mchezo huo.
Katika mchezo wa awali, Manchester United walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Huddersfield, huku staa mpya wa timu hiyo, Alexis Sanchez akiifungia timu yake bao moja likiwa ni la kwanza kwake kuanzia ajiunge nayo akitokea Arsenal.
Bao lingine la United liliwekwa kimiani na Romelu Lukaku, huku Manchester City wao wakitoka sare ya bao 1-1 na Burnley.
TANO Z IJAZO ARSENAL
Tottenham -UGENINI- Feb 10
Ostersund -UGENINI- Feb 15
Ostersund -NYUMBANI- Feb 22
Man City -UGENINI- Feb 25
Man City -NYUMBANI- Mar 1
Arsenal: Cech (Ospina 69), Bellerin, Koscielny, Mustafi, Monreal (Kolasinac 45), Ramsey (Wilshere 74), Xhaka, Mkhitaryan, Ozil, Iwobi, Aubameyang.
Subs: Lacazette, Chambers, Maitland-Niles, Elneny.
Scorers: Ramsey 6, 19, 73, Koscielny 14, Aubameyang 37
Booked: Koscielny, Mustafi
Everton: Pickford, Keane (Davies 45), Williams, Mangala, Kenny, Schneiderlin, Gueye, Martina, Walcott (Calvert-Lewin 60), Niasse (Tosun 77), Bolasie.
Subs: Rooney, Tosun, Sigurdsson, Holgate, Robles.
Scorers: Calvert-Lewn 64
Referee: Neil Swarbrick
No comments:
Post a Comment