Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi amekiri kuwepo kwa mgogoro wa wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) eneo la Kisakasaka.
Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Jimbo la Dimani Juma Ally Juma aliehoji Kuna mgogoro wa kati ya Jeshi la polisi na wananchi wa Kisakasaka hali iliyoleta wasiwasi kwa wananchi, Je? ni lini serikali itapatia ufumbuzi wa mgogoro huo?
“Ni kweli kwamba mgogoro huu ni wa muda mrefu nataka nimfahamishe Mh. Juma kwamba mimi binafsi nimefika eneo hilo nilifanya mazungumzo na uongozi wa kikosi pamoja na uongozi wa eneo pamoja na wananchi wa pale kulizungumza na kama nilivyosema kwenye swali langu la msingi inachokwamisha kutatua sasa hivi ni suala la fedha za kupima kwasababu jeshi lilisharidhia kufanya mabadiliko ya mipaka yake ili wananchi wanaoonekana ndani ya kambi waweze kutolewa lakini .Hata hivyo nitazungumza na Mh. Mbunge ili kumueleza zaidi ni hatua gani zinazostahili kuchukuliwa kwa mujibu wa ziara niliyoifanya pale na fedha zikipatikana,” amesema Waziri Mwinyi.
No comments:
Post a Comment