KUFUATIA skendo nzito inayofukuta ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutoka kimapenzi na warembo, Wema Isaac Sepetu na Tunda Sebastian, mama mzazi wa mwanamitindo Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga ‘amemtapika’ jamaa huyo kuwa vitu vyote vinavyoendelea kwenye mitandao ya kijamii havihusiani na mwanaye.
Akizungumza na gazeti hili, mama Mobeto alisema kuwa, kwa sasa, kwa upande wao, yeye na mwanaye Mobeto hawataki malumbano na kuwekana kwenye mitandao wa kijamii ndiyo maana hawataki kusikia habari zinazomhusu Diamond.
Alisema kuwa, muda huo wa malumbano hawana kwa sababu mwanaye anaendelea na maisha yake mengine kabisa ya kutafuta maendeleo na jinsi gani ya kuwalea watoto wake na si kumtegemea mwanaume huyo.
“Jamani sisi mambo hayo ya kwenye mitandao muda huo hatuna tena. Hata mtoto wangu (Mobeto) ameshayasahau mambo hayo na badala yake yupo bize na mambo yake mengine kabisa,” alisema mama Mobeto.
Mama Mobeto aliendelea kueleza kuwa, mtoto wake yuko kwenye mchakato mkubwa wa kufungua biashara yake ya lipstiki hivyo muda wa kufuatilia chochote kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii hana.
“Michakato yetu sisi zaidi ni kutafuta pesa na si vingine. Muda wa kuchokonoana kwenye mitandao hatuna kwa sababu tukifanya hivyo hatuwezi kupiga hatua hata siku moja, lakini kama kuna watu wanaweza kufanya hivyo, wafanye kwani sisi tulishajivua siku nyingi sana na wala hatutaki kumsikia huyo Diamond na mambo yake,” alisema mama Mobeto.
No comments:
Post a Comment