Wakulima wa Kata ya Kiberege Wilayani Kilombero mkoani Morogoro, wamejikuta katika wakati mgumu, baada ya mazao yao kuvamiwa na panya waharibifu, na kusababisha uharibifu mkubwa katika mazao ya mpunga na mahindi ambayo wameyapanda katika msimu huu.
Wakulima wa kata hiyo wamesema tatizo hilo limeanza kwa muda mrefu, na cha kushangaza licha ya mvua kunyesha bado panya hao wameendelea na uharibifu, hali ambayo inawapa mashaka juu ya hali ya chakula itakavyokuwa msimu huu.
Aidha wakulima hao kutoka katika vijiji vya Nyamwezi na Misufini, wamedai ndiyo mara ya kwanza kuwanaona panya hao wakiharibu mazao yao.
Naye Afisa Kilimo wa Kata ya Kiberege amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na ameeleza kuwa Serikali ya Wilaya hiyo imeanza kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakabiliana na tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment