St Louis ya Shelisheli
WAKATI wakiwa wanajiandaa kuvaana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi wa klabu ya St Louis ya Shelisheli umeanza mchecheto.
Timu hiyo inakuja nchini kucheza na Yanga Febrauri 11, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar. Meneja wa St Louis, Davis Khan aliidai kuwa; “Kucheza michuano hii wakati ligi yetu imeisha kunachangia sisi kufanya vibaya tena ukiangalia wapinzani wetu wao wanaendelea kucheza na wanashinda katika michezo yao migumu.”
Yanga wakiendelea na mazoezi yao.
“Pia katika wakati huu tunasaka kocha mwingine baada ya yule wa awali kujiuzulu, ambapo kocha huyo atakuwa na muda mdogo sana kabla ya kucheza kwa mchezo wetu huo na Yanga, ila tunajaribu kuwa na mtu haraka iwezekanavyo,” alisema Khan kupitia kwenye moja ya mitandao ya nchini kwao.
St Louis watacheza na Yanga kwenye michuano hiyo baada ya kuwa mabingwa wa Ligi ya Shelisheli ambayo ilimalizika mwezi Novemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment